IWAPO UMEANZISHA THREAD (UZI) JAMIIFORUMS, NA THREAD YAKO IKATIWA KAPUNI NA MODS. JIBU LAKO LIPO KWENYE BLOGU HII. TUPIA UZI HUO ILI TUUWEKE OPENLY TUPIA KWA EMAIL: jamiiforumsblog@gmail.com

Wengine Wanasemaje?

Sunday, July 29, 2012

SMS KALI ZA MAPENZI

Wakuu wa Jukwaa La Malavedave;

Bila ya shaka wengi mmewahi kutuma au kupokea SMS za Mapenzi kuhusiana na subject mbalimbali katika mapenzi. Hata hivyo kuna zile ambazo zinafurahisha sana na pia kutia raha mara ukisoma. katika hizo chache nilizokutanaza nazo. Naomba, usome, tafakari, cheka, kisha na wewe tuambie ni SMS gani ulizokutana nazo ambazo ukizikumbuka zinakufurahisha?

  • Najiuliza kila leo hivi ni mimi tu kimeo katika dunia hii ya leo maana kila leo nayempata huishia kunipa ahadi kila leo, mpenzi kila siku waniaidi mara nitakupa leo mara kabla ya machweo, hivi ni lini utanipa jibu la uhakika nakunipa mapenzi ya uhakika nipate farijika? Nakupenda mpenzi.

  • Kila siku najiuliza moyoni hivi ni nini nilichokukosea jamani? Mitaani sikuoni, hata njozini pia huonekani hivi kweli upo hapa duniani? Naamini nitapata kusikia toka kwako siku za usoni,nimekumiss nakueleza toka moyoni, zaidi kumbuka haya siyo maisha wanayoishi marafiki duniani!

  • Hakika mtoto umeumbika mithili ya malaika japo mbinguni sijafika lakini nauhakika kwa kila mwanaume aliyeumbika na kukamilika akikuona lazima udenda utamtoka, naomba japo yako dakika nipate kukueleza moyoni yaliyonifika kwani siwezi tena kuficha jinsi navyokupenda, nakupenda amini kwako nimefika!

  • Nakupenda dear, amini moyoni umeniingia ndiyo maana mimba nikaamua kukubebea pasipo kunioa hakika mahaba yako yanifanya nijione malkia katika hii dunia! Nakupenda

  • Ukweli lazima nikwambiye kwa kuwa sina kimbilio nakupenda kijana mwenzio sijui kwanini hutaki kukisikia changu kilio, namwomba Mungu kila kukicha usikiye changu kilio, nakupenda na kama kukueleza hili nakukosea nisamehe kwani si langu kusudio,luv u mwaah.
Je, Ni SMS gani za kufurahisha za mapenzi umewahi kukutana nazo? share with us with a light touch.

Peace and Love.

Respect

mdau

1 comments:

Tengelimale said...

maada tamu sana inaheat

Post a Comment