Kwa mujibu wa magazeti ya Tanzania Daima na Mtanzania, waliotajwa katika orodha hiyo ni :
- Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli
- John Samwel Malecela
- Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Philip Mangula
Majina hayo yanaongezea idadi ya majina aliyoyataja Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambapo ni:
- Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali
- Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
- Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
- Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina
- Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa
- Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge
- Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
- Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
- Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM)
- Rais mstaafu, Benjamin Mkapa
- Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete
Ikaelezwa kuwa, Malecela na Mangula wameongezwa kwenye orodha kwa kuwa walitoa maagizo kupitia 'memo' zilizofanikisha wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA, kupitia Benki Kuu; wakati Dk. Magufuli kashifa iliyomwingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa ufisadi, ni ya uuzaji wa nyumba za Serikali ambazo ziliuzwa kwa watu wasiostahili na nyingine hazikutakiwa kuwekwa sokoni.
Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye anatajwa "kuhusika" kwa kuwa alikuwa Waziri Mkuu na alifahamu kilichokuwa kikiendelea lakini akaamua kunyamaza kimya. Gazeti la Majira limenukuu msemaji wa CHADEMA wakisema kwamba Sumaye hakutajwa kuwa "ni" au "si" mmoja wa waliopo kwenye orodha ya watuhumiwa wa ufisadi.
Nape akataarifu yaliyosemwa na Dk. Slaa kuwa, ”Huo ni sawa na mchezo wa kuigiza. Hatua hiyo haina lolote katika mchakato wa kung'oa mafisadi ndani ya chama chetu tena nawaambia wanachofanya ni sawa na kuwasha moto juu ya petroli... bahati nzuri tumeshajua mipango yao yote ya kujaribu kuendesha kampeni ya kuchafua watu wasafi ndani ya chama akiwamo Rais na familia yake... Tunajua wamepanga kutumia baadhi ya vyama vya siasa vya upinzani, viongozi wa dini, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi. Kwa hiyo hata hiyo orodha mpya tunajua ni sehemu ya mchezo huo."
“CCM ni chama kikongwe, hatufanyi kazi kwa kuwaiga CHADEMA kwa sababu Chadema hawawezi kusema hiki leo na sisi kesho tunawafuata, haiwezekani, ngoja waendelee. Hao CHADEMA hawawezi kutuchagulia mchafu ni yupi na msafi ni yupi, waache waendelee na kama wana orodha yao nyingine, waendelee kutaja."
0 comments:
Post a Comment