IWAPO UMEANZISHA THREAD (UZI) JAMIIFORUMS, NA THREAD YAKO IKATIWA KAPUNI NA MODS. JIBU LAKO LIPO KWENYE BLOGU HII. TUPIA UZI HUO ILI TUUWEKE OPENLY TUPIA KWA EMAIL: jamiiforumsblog@gmail.com

Wengine Wanasemaje?

Saturday, May 12, 2012

ORODHA YA WATUHUMIWA WA UFISADI TANZANIA

Baada ya Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, kuyataja majina aliyosema ni ya wanatuhumiwa wa ufisadi nchini Tanzania, katika mkutano wa hadhara mkoani Tabora magazeti ya MwananchiNipashe na Mtanzania yana ripoti kuwa Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Zanzibar amesema, “...yaliyosemwa Tabora na Dk. Slaa, ni hila za hao hao wenye shutuma za ufisadi lakini sisi tumejipanga vizuri wasijidanganye kuwa tutarudi nyuma, tutahakikisha chama kinakuwa safi na wenye shutuma wakafanye shughuli nyingine.”

Kwa mujibu wa magazeti ya Tanzania Daima na Mtanzania, waliotajwa katika orodha hiyo  ni :


  1. Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli 
  2. John Samwel Malecela
  3. Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, Philip Mangula

Majina hayo yanaongezea idadi ya majina aliyoyataja  Septemba 15, 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam ambapo ni:

  1. Gavana wa Benki Kuu (BoT), Marehemu, Dk. Daudi Balali
  2. Mbunge wa Bariadi, Andrew Chenge (CCM)
  3. Basil Mramba aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Rombo (CCM) na Waziri
  4. Gray Mgonja aliyekuwa Katibu Mkuu mstaafu, Hazina
  5. Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Patrick Rutabanzibwa
  6. Nazir Karamagi aliyewahi kuwa Mbunge
  7. Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono (CCM)
  8. Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz (CCM)
  9. Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM)
  10. Rais mstaafu, Benjamin Mkapa
  11. Rais wa Sasa, Jakaya Kikwete

Ikaelezwa kuwa, Malecela na Mangula wameongezwa kwenye orodha kwa kuwa walitoa maagizo kupitia 'memo' zilizofanikisha wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje, EPA, kupitia Benki Kuu; wakati Dk. Magufuli kashifa iliyomwingiza kwenye orodha ya watuhumiwa wa ufisadi, ni ya uuzaji wa nyumba za Serikali ambazo ziliuzwa kwa watu wasiostahili na nyingine hazikutakiwa kuwekwa sokoni.

Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye anatajwa "kuhusika" kwa kuwa alikuwa Waziri Mkuu na alifahamu kilichokuwa kikiendelea lakini akaamua kunyamaza kimya. Gazeti la Majira limenukuu msemaji wa CHADEMA wakisema kwamba Sumaye hakutajwa kuwa "ni" au "si" mmoja wa waliopo kwenye orodha ya watuhumiwa wa ufisadi.

Nape akataarifu yaliyosemwa na Dk. Slaa kuwa, ”Huo ni sawa na mchezo wa kuigiza. Hatua hiyo haina lolote katika mchakato wa kung'oa mafisadi ndani ya chama chetu tena nawaambia wanachofanya ni sawa na kuwasha moto juu ya petroli... bahati nzuri tumeshajua mipango yao yote ya kujaribu kuendesha kampeni ya kuchafua watu wasafi ndani ya chama akiwamo Rais na familia yake... Tunajua wamepanga kutumia baadhi ya vyama  vya siasa vya upinzani, viongozi wa dini, baadhi ya vyombo vya habari na waandishi. Kwa hiyo hata hiyo orodha mpya tunajua ni sehemu ya mchezo huo."

“CCM ni chama kikongwe, hatufanyi kazi kwa kuwaiga CHADEMA kwa sababu Chadema hawawezi kusema hiki leo na sisi kesho tunawafuata, haiwezekani, ngoja waendelee. Hao CHADEMA hawawezi kutuchagulia mchafu ni yupi na msafi ni yupi, waache waendelee na kama wana orodha yao nyingine, waendelee kutaja."

0 comments:

Post a Comment