IWAPO UMEANZISHA THREAD (UZI) JAMIIFORUMS, NA THREAD YAKO IKATIWA KAPUNI NA MODS. JIBU LAKO LIPO KWENYE BLOGU HII. TUPIA UZI HUO ILI TUUWEKE OPENLY TUPIA KWA EMAIL: jamiiforumsblog@gmail.com

Wengine Wanasemaje?

Wednesday, August 1, 2012

HOTUBA YA KIKWETE TAR. 01 AUGUST 2012

Wana JF

Rais Kikwete leo saa kumi kamili jioni anazungumza na taifa kupitia kwa wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari Ikulu jijini Dar. Agenda kuu iko mfukoni mwake, lakini swala la mgomo wa walimu huenda likatawala mkutano huo.

MY Take: JK akumbuke kuna kesi maakamani na hukumu inatolewa kesho. Mkutano wake usije ukaingilia uhuru wa mahakama na kuathiri maamuzi ya kesho.

Updates:

Jamani anayefuatilia mkutano huu kwa Radio ama TV atoe updates hapa mara utakapoanza. Mie nitajaribu kutoa updates kama bepari wangu akinipa upenyo kidogo.

1) Anazungumzia maswala kuhusu uchimbaji na utafutaji gesi asilia na sheria zihusuzo sekta ya gesi

2. Anaongelea waalimu sasa, kuwa serikali inawajali na inawathamini sana, ila mengi yataongelewa kesho na mahakama

3) Anasema madai ya walimu ni makubwa na serikali haina uwezo wa kutoa mishahara kiasi hicho

4) Anasema hawapuuzi walimu ila madai yao ni magumu kutekelezwa. Abeza pia kuipelekea notisi serikali ijumaa wakati jumamosi na jumapili ni siku za mapumziko

Maswali now;
Kibanda anauliza; Serikali imejifunza nini kufuatia migomo kuendelea?
Serikali bado inatuhumiwa kuhusika na utekwaji ulimboka, nini kauli yake??

MAJIBU; CT SCAN sio sawa na shangingi moja, anayesema hiyo ndio bei ya CT scan aende akapewe pesa ili alete hiyo CT scan.

Swali la Pili: Bakari Machumu -Citizen; Kuhusu serikali kuwashirikisha wadau wengine katika sekta ya nishati na hasa gesi.

MAJIBU: Serikali inawashirikisha na inafanya jitihada za kuwa karibu na wote wanaosaidia katika sekta za nishati, gesi na uzalishaji umeme hadi hali itakapokuwa nzuri. Kubinafsisha Tanesco bado si muafaka ila mambo mengine yatafanywa na watawala wajao 2015

Swali la Tatu: Jesse Kwayu Nipashe; Kukithiri kwa rushwa katika sekta mbalimbali, jitihada gani zimefanywa na serikali maana bado Rushwa inazidi kukithiri ikiwa ni pamoja na wabunge kuanza kuhusishwa na rushwa pia.
MAJIBU: Rais peke yake hawezi kupambana na rushwa ila mfumo mzima. Serikali imejitahidi kuboresha sheria ya rushwa na kuongeza makosa ya rushwa, PCCB ina ofisi hadi wilayani na ina watumishi wa kutosha, hii ni kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa kupambana na rushwa.

Swali la Nne: Kuhusu uporaji ardhi, na namna serikali inavyolinda ardhi na hasa katika swala la ushirikiano wa jumuiya ya Afrika mashariki
MAJIBU: TIC na Serikali za vijiji ndio wanaoweza kugawa ardhi na serikali itaendelea kulinda ardhi inufaishe wazawa.

PRESS CONFERENCE IMEKWISHA

0 comments:

Post a Comment